Music: Fredrick Albert Komba
Lyrics: Fredrick Albert Komba
MoroBuzz Season 3 ep 1 lyrics
Piga Makofi
Piga nduru kama vile umekabwa
Piga nduru kama tonge limekwama
Demu ama jamaa akileta drama
Sipotezi muda nashika tu simu block
Huu sio muda wa kutavutana
Nina vitu vya kuvuta sio marijuana
Nafanya nachopenda kwa bidii sana
Nivute mikwanja nimpelekee Mama
Home wanasali nitusue
Kidogo matofali nifyatue
Wachawi wanataka wanipangue
Kipindi Sir God amenipa duet
Piga makofi piga makofi, piga makofi tafadhali
Piga makofi piga makofi, hata usipopiga mi sijali
Piga makofi piga makofi, kama ndoto zako ni kufika mbali
So upige makofi usipige makofi, makofi yako hayanikoseshi ugali
Mi napiga mishe nijaze matenga
Studio kila siku najaza mabenga
Nimebeba Bongo nzima kwa mabega
Kipenzi cha watoto mpaka mabazenga
Wakati mna rehearsal kufanya playback
Siku nikishika stage mtakuja learn kwamba
Vile nitakavyopeleka hii climax
Itabidi mrudi darasani mka learn kwanza
Nasoma kila siku ili nikue
Mchezo nikiushika niubutue
Siri nimeipata vipi niifichue?
Bora kunyamaza acha niuchubue