Lyrics: PAUL THIMOS MWASILE/BONVENTURE ELIUTER KABOGO Music: PAUL THIMOS MWASILE/BONVENTURE ELIUTER KABOGO Intro Yeeeeyehh/ Aaaah/ Toa ndugu/ Anakuona/
Verse 1 Eeh!kama nina nguvu ya kutafuta siwezi ita mtu Tajiri/ Tajiri sio kipaji ni kazi nguvu na akili/ Tatizo tukipata pesa tunapoteza marafiki/ Harafu tunapata wapambe ambao hatukuwa nao kwenye dhiki/ Neno la ufahamu ni lile neno lenye elimu/ Ila neno lenye utamu ni lile lililotiwa ndimu/ Japo wengi hawafahamu tofauti ya hamu na stimu/ Kama ilivyo tofauti ya maarifa na elimu/ Kipindi unamtongoza demu ili uonekane mjanja/ Mi namtongoza dalali ili nipate kiwanja/ Harafu sasa,ukipaka mkongo umkomoe mchumba/ Mwezako niko site ndio naipaka rangi nyumba/ Eeh! Tusibishane kuhusu hili kuna vichwa viwili/ Ila cha chini hakifikiri/ Mwanume aliyevaa vikuku aliyetoga masikio na pua/ Huyo mwanaume sie hatuhusu sio mwanaume tunaemjua/ Maskini wenge tuna ndoto za utajiri kichizi/ Hazitimii sababu tunastuka katikati ya usingizi / Hatujakuzwa kuamshwa na alarm ili tuamke/ Tunaamshwagwa na shida Tuache shuka tukatafute/
Chorus Toa ndugu ,toaaaa(toa ndugu) Toa ulicho nacho (ulicho nacho) Bwana anakuona(anakuona) Mpaka moyoni mwako x2
Verse 2 Acha nikwambie/ Kuna urithi wa aina mbili/ Kuna urithi wa mali na ule urithi wa akili/ Urithi wa mali,utakupa mali za utajili/ Ila urithi wa akili unaweza usikupe akili za dili/ Na kwenye Maisha/ Maisha hayaishi sababu yako Ila wewe ndio unasababu ya kuishi kivyako / So kabla ya kuvuta ganja hakikisha unavuta pumzi/ Maana pesa ni mwanamke ambae abaki kama umtunzi/ Na kwenye ukoo sina ndugu yeyote Tajiri/ Na kama yupo basi lazima awe mbahiri/ Mungu anables adoado najikongoja/ Na ghetto nikiishiwa gesi nawasha data naunga mboga/ Mama angu pekee ndiyo mwanamke nae mwamini/ Japo nae alirubuniwa ndiyo nikapatikana mimi/ Peace kwa wanawake wote kima cha chini na juu/ Nawapa mimba za fikra msimeze p2/ Mambo madogodogo hayo nitawapa haina kwele/ Siwezi kuwapa nyumba labda nyumba za milele/ Na kuhusu kupush mtapush mkipata mimba/ Kwa hiyo ni udhushi nikisema mtapush ndinga/ Chorus Toa ndugu ,toaaaa(toa ndugu) Toa ulicho nacho (ulicho nacho) Bwana anakuona(anakuona) Mpaka moyoni mwako x2
Hook Usifanye moyo wako kuwa mgumuu wewe….. Toa ulicho nacho huende bwana anakuona….