Lyrics: Philbert Afred Music: Frankin Nhcimbi Uzuri sio sura dada ooh wala uzuri sio shape yako mwanamke mwanamke kaumbwa na haya mwanamke kuwa na stara mambo wajiamulia,shule hutaki sikia Kutwa kwenye tekinolojia Hutaki ushauri,tena wadai umekua
na mama alikufunda binti maringo nenda polepole Usijifanye wewe bingwa wa mapenzi Dunia ni shule itakufundisha oooh
maringo binti maringo tena ujituunze daima *2 Dunia haikupi nafasi mara mbili (aah dada pole) chunga dada usilambe shubiri (aah dada pole) walimwengu watakusifia kesho watakushusha (aah dada pole) Ooh dada dunia haikusubiri
chunga roho ooh roho yako roho isiwe na tamaa watakupa maporoso uanze madoido, madoido yatakuumbua dada Dunia ni pori miluzi mingi itakupoteza Kwa sifa na story watakujaza ujae Oooh ooh
na mama alikufunda binti maringo nenda polepole Usijifanye wewe bingwa wa mapenzi dunia ni shule itakufundisha ooh