Lyrics: Goodluck Gozbert/Timothy Boikwa Music: Goodluck Gozbert/Timothy Boikwa Nimeona Majina Makubwa, kupita Yote Ila katika Hayo langu lilikua juu Nimeona Magari mazuri ya dunia hii Tena katika hayo langu Lilikuwa Juu Nikaona Yaliyo mafanikio nyingi Baraka Tena katika hizo zangu zilikua
Wacha nikueleze patano langu na Mungu Napitishwa hapa Ananipeleka Juu Ukionaninapumua bado Misuko suko ni kama zoezi Sichanganywi na Ripoti ya Leo Mchicha Bamia sio Sukuma wiki Najizungusha nikingojea Nyama Bado Sijakamilika Ninatayarishwa
Ukiweza Nihukumu nikiwa na hali ngumu Ila ungalijua ungekaa kimya Alinipaka mafuta nitawale Nami nasubiri Baraka zangu niketi enzini Sawa Nimezidi mikopo madeni ya kila duka Hao ni maajenti wa Kampuni Yangu Ya Baadae Ninabariki wenzangu Maana Nimebarikiwa Sina laana Kwanini Niwachukie Eh Ninaombea wenzangu Wafanikiwe Wajue, Ndivyo Tulivyo washindi
Wacha nikueleze patano langu na Mungu Napitishwa hapa Ananipeleka Juu Ukionaninapumua bado Misuko suko ni kama zoezi Sichanganywi na Ripoti ya Leo Mchicha Bamia sio Sukuma wiki Najizungusha nikingojea Nyama Bado Sijakamilika, Ninatayarishwa