Music: Ambrose Akula Akwabi/Kevin Omondi Okech
Lyrics: Fredrick Mulla
Ukiniona unanuna unafura huna furaha
Mi nazidi nenepa natuna natuna
Unapaka vibaya kwa watu mi ni mbaya
Wakae mbali nami cha ajabu wanazidi sogea
Mwenye roho ya korosho ni nani sasa
Kati yangu mimi na wewe mchawi nani sasa
Najua unanichukia lakini inabidi uzoeange
Najua hunipendi ukiniona unavimba uzoeange
Najua unanichukia lakini ukiniona uzoeange
Najua hunipendi ukiniona unavimba uzoeange
Itabidi unizoee nasonga mbele sio nyuma nana
Upendo ndio nguzo we yanini vijembe na kufarakana
Ila kama unalipwa rupia kuja nisengenya
Endelea tuone nani atashinda
Mwenye roho ya korosho ni nani sasa
Kati yangu mimi na wewe mchawi nani sasa
Najua unanichukia lakini inabidi uzoeange
Najua hunipendi ukiniona unavimba uzoeange
Najua unanichukia lakini ukiniona uzoeange
Najua hunipendi ukiniona unavimba uzoeange
Wewe zidi na wivu wako we
Mi nakuombea dua dua
Najua hunipendi mwana wa mwenzio
Sitachoka kukuombea dua dua na unajua