Music: Abisay hizza
Lyrics: Abisay hizza
Story ya maisha yangu kwa kifupi mi nakupa
Jinsi ilivyokuwa huu wokovu nikapata
Sio mpango wa mungu watu wengi wanahisi
Kumleta mrembo malkia sio rahisi
Sikiliza nikusumbue ilivyokuwa ndugu yangu
Siku moja maskani nimechill na wanangu
Alipita mrembo mnyamwezi nikaunga tela
Nikaanza kumsemesha huku nikimwaga sera
Kanikatia juu juu na hilo jibu shindwa
Sikukata tama kesho yake nikadamka
Nikaanza fuatilia wapi anatokea wapi anaelekea
Nilikata tamaa nilipoona kanisani kivipi niwe naye
Na yeye ni msafi kwanzia matendo sura mpaka tabia
Kichwa chini nikaondoka huku nikimfikiria.
Nawaza kwa kina juu ni upendo
Wa namna gani
Utafanya chochote ili mimi
Nikuamini
Ivi upendo maana yake ni nini?
Mungu anajua maana yake ni nini
Utata unakuja usiku nikilala ni yeye namuotea
Yu karibu nami na ni tenzi ananiambia
Mara ananiombea mara ananiambia
Yesu anaokoa
Stori za biblia ndugu yangu ndio usipime
Story ya mwisho ilikuwa ya paulo mtume
Jumapili nakurupuka kanisani najiandaa
Majamaa wanashangaa nilivyovaa
Suruali ya kitambaa nimepasi imenyooka
Chini mepiga moka ndio mtoko niliotoka
Kanisani siti ya mbele karibu na wanakwaya
Lengo langu aninone ye sianaimbaga kwaya
Hazikupita week mbili nikajiunga na kwaya
Taratibu taratibu injili nikaipokea
Sikuamini mimi kama yesu ningempokea
Mungu wa ajabu.
Ivi upendo maana yake ni nini?
Mungu anajua maana yake ni nini
Ivi upendo maana yake ni nini?
Mungu anajua maana yake ni nini
Amini usiamini mungu anakupenda
Hivyo atatumia njia yeyote ili kukuokoa
Na ukiamini chochote kinaweza kuwa.